Chanzo cha kidonge cha tiba ya vidonda vya tumbo kutumika kuavya mimba duniani

Misoprostol

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni suala ambalo mara nyingi husababisha mgawanyiko mkubwa katika nchi nyingi, na bado ni marufuku katika baadhi ya nchi hizo: utoaji mimba.

Suala hili pia linaathari kubwa kwa maisha ya mamilioni ya wanawake.

Na wale wanaoamua kuavya mimba wanaweza kufanya hivyo kupitia njia mbili kuu: utoaji mimba wa matibabu au upasuaji.

Utoaji mimba wa upasuaji unahusisha operesheni ya kuondoa kijusi kutoka kwenye nyumba ya uzazi.

Utoaji mimba kupitia upasuaji inajumuisha oparesheni ya kutoa mimba kutoka kwenye nyumba ya uzazi.

Lakini Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema ikiwa dawa ya mifepristone haipatikani pia misoprostol inaweza kutumiwa peke yake.

Dawa hii hata hivyo haikuundwa kwa ajili ya kutoa mimba. Ilitengenezwa kwa ajili ya kutibu vidonda vya tumbo na iliingizwa kwenye soko kwa jina la Cytotec katikati ya miaka ya -1980.

Na ni wanawake wa Amerika Kusini ambao walikuwa wa kwanza kugundua matumizi yake mengine na uwezekano wa dawa hiyo kutumiwa kwa uavyaji mimba.

"Matumizi mengine ya dawa hii ilivyoenezwa"

"Hii ilitokea katika miaka ya 1980 na wanawake, ambao ni wazi walikuwa na rasilimali kidogo, walianza kutambua kwamba dawa ambayo ilitengenezwa kutibu idonda vya tumbo hatimaye ilisababisha kutengana kwa nyumba ya uzazi," Dkt. Georgina Sánchez Ramírez aliiambia BBC Mundo, mwandishi wa "Realities and Challenges of Medication Abortion in Mexico"

"Kwa njia hii kama kawaida, watu walianza kunong'onezana na hatimaye gumzo likaibuka kuhusu uwezekano wa dawa hii kutoa mimba. Na kwa kweli gharama sio kubwa kwa sababu ilitengenezwa kwa ajili ya kutibu vidonda vya tumbo," anasema mtaalamu wa Jinsia na Afya wa chuo cha Frontera Sur huko Mexico.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Cytotec (misoprostol) ilitengenezwa na kampuni ya dawa ya Searle katikati ya miaka ya 1980.

Misoprostol ilitengenezwa mwaka 1973 na watengenezaji dawa wa Searle na ingawa awali iliingizwa sokoni kama dawa ya kukabiliana na matatizo ya tumbo, ilibainika kuwa moja ya athari zake ilikuwa ni kuharibu mimba.

Mwishoni mwa miaka ya 1980, kama suluhu kwa Brazili kuharamisha uavyaji mimba, wanawake walianza kupendekeza dawa hiyo, kisha kuuzwa bila agizo la daktari, ili kutoa mimba.

Mwaka 1987, watafiti nchini Ufaransa walitengeneza mifepristone mahasusi kwa ajili ya kuavya mimba, na dawa hii, ikichanganywa na misoprostol, ilionyeshwa kuwa njia nzuri sana ya kutoa mimba.

Lakini kufikia wakati huo, wanawake huko Amerika Kusini, ambako utoaji-mimba uliharamishwa katika nchi nyingi, walikuwa wakitumia sana misoprostol, kama Dkt. Sánchez Ramírez anavyoeleza.

"Kabla ya mifepristone kutengenezwa katika maabara nchini Ufaransa, huko Amerika ya Kusini baadhi ya wanawake tayari walikuwa na taarifa ikiwemo ni kipimo gani na jinsi ya kutumia dawa ambayo awali ilitengenezwa na inaendelea kutumika kutibu vidonda vya tumbo," anasema mtaalamu huyo.

Jinsi dawa hii inavyofanya kazi

Utoaji mimba wa matibabu hauhitaji utaratibu wa upasuaji na, mara nyingi, unaweza kufanywa nyumbani.

Mchanganyiko wa mifepristone na misoprostol kawaida hutumiwa.

Kidonge cha kwanza kumezwa ni mifepristone, ambayo huzuia homoni ya progesterone ambayo mwili unahitaji ili mimba iendelee kukua.

Dawa ya pili, misoprostol, inamezwa saa 24 hadi 48 baadaye. Saa chache baada ya kumeza dawa hii, nyumba ya uzazi huvunjika, na kusababisha maumivu, kutokwa na damu, na hatimaye kutoka kwa mimba.

Pia unaweza kusoma:

WHO inasema ikiwa mifepristone haipatikani, basi misoprostol inaweza kutumiwa peke yake.

Kama Dkt. Georgina Sánchez Ramírez anavyoonesha, katika nchi au mahali ambapo uavyaji mimba ni kinyume cha sheria, uuzaji wa mifepristone umepigwa marufuku. Lakini hata pale ambapo ni halali, misoprostol inatumika sana.

"Kwa kuwa mifepristone imeainishwa kama dawa ya kipekee ya kukatiza ujauzito, si rahisi kuipata kwa sababu, kwa hakika, ni sehemu ya marufuku (ya kutoa mimba) ambayo kila moja ya majimbo au miji inayo," anasema Sánchez Ramírez.

"Na hata katika maeneo ambayo utoaji mimba umeharamishwa, kama vile Mexico City, tuna marejeleo kutoka kwa watumiaji ambao wanaonesha kuwa mifepristone haiuzwi katika maduka ya dawa katika maeneo haya na pia gharama yake ni ya juu."

"Ndiyo maana misoprostol inatumika kwa wingi zaidi, pamoja na kuwa nafuu," anaongeza.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Katika miaka ya 1980 iligunduliwa kuwa mifespristone, pamoja na misoprostol, ilikuwa njia nzuri sana ya kushawishi uavyaji mimba.

Uavyaji mimba wa kimatibabu sasa unachangia sehemu kubwa ya utoaji mimba wote unaofanywa ambapo utaratibu huo ni halali.

Nchini Marekani, kwa mfano, zaidi ya nusu ya utoaji-mimba wote unaofanywa ni utoaji-mimba wa kitiba.

Zaidi ya hayo, tafiti zinaonesha kuwa kuongezeka kwa utoaji mimba wa kimatibabu sio tu kumeruhusu wanawake wengi zaidi kupata nafasi ya kuavya mimba kwa hiari, lakini pia kumepunguza kwa kiasi kikubwa vifo na matatizo yanayotokana na uavyaji mimba wa kisiri.

Kadhalika, utoaji mimba wa kimatibabu pia umeondoa vizuizi ambavyo mara nyingi vilichelewesha mchakato, na kuruhusu uavyaji mimba kufanyika nyakati ambazo ni salama.

Lakini kama vile Dkt. Georgina Sánchez Ramírez anavyoosema, pengine jambo muhimu zaidi ni kwamba upatikanaji wa dawa za kuavya mimba huwapa wanawake utaratibu wa faragha zaidi na usiovamizi na huwaruhusu kupata na kutumia dawa hiyo bila kuingiliwa na mtaalamu wa matibabu. mhudumu wa afya.