Kwa nini Urusi haikuweza kushikilia Kisiwa cha Snake

Urusi ilidai kuwa Ukraine ilizindua ombi lililofeli la kukamata tena kisiwa hicho lakini Uingereza inasema vita bado haijaisha

Chanzo cha picha, PLANET LABS PBC

Maelezo ya picha,

Urusi ilidai kuwa Ukraine ilifanya shambulio lililofeli la kukomboa tena kisiwa hicho lakini Uingereza inasema vita bado haijaisha

Sehemu hii ndogo ya mawe kaskazini-magharibi mwa Bahari Nyeusi ilitekwa na Urusi katika siku ya kwanza ya uvamizi wake wa Ukraine, na imekuwa na jukumu kubwa katika vita tangu wakati huo.

Baada ya zaidi ya miezi minne ya mashambulizi ya mara kwa mara ya Waukreni, vikosi vya Urusi vimekiacha Kisiwa cha Snake, au Kisiwa cha Zmiinyi kama kinavyojulikana nchini Ukraine.

Urusi inasema kuwa imeondoa wanajeshi wake kama "ishara ya nia njema" kuthibitisha kuwa haizuii uuzaji wa nafaka nje, lakini Ukraine ilipuuza madai hayo, huku Moscow ikiendelea kushambulia kwa makombora maduka yake ya nafaka.

Vigumu kutetea

Kisiwa hicho kinakabiliwa na mashambulizi kutoka pande zote kutoka angani na baharini, na kikosi kidogo cha askari waliopewa jukumu la kukilinda - kwanza Waukraine na baadaye Warusi - wameelezewa kama "bata waliokaa" na wataalamu wa kijeshi.

Kisiwa cha Nyoka kiko kilomita 35 kutoka pwani ya Ukraine - na kilitekwa na Warusi mnamo Februari 24ndani ya safu ya makombora, mizinga na droni kutoka ufukweni.

Na wanajeshi wa Ukraine wamefanya hivyo, wakidai msururu wa mashambulizi mabaya kwenye kisiwa chenyewe na chombo chochote kinacholeta askari na silaha nzito.

Mnamo Aprili, uwezo wa Urusi wa kupambana na ndege katika Bahari Nyeusi eneo la kaskazini-magharibi ulidhoofishwa sana baada ya meli yake kubwa Moskva kuzama kwenye Bahari Nyeusi.

Hiyo inaeleza kwa nini Kremlin ilikuwa na hamu kubwa ya kuleta mifumo ya kuzuia ndege na vita vya kielektroniki vya redio kwenye Kisiwa cha Snake. Lakini mambo hayakuenda kama ilivyotarajia kwa sababu ilikuwa mbali sana na kambi zake kuu za baharini katika Bahari Nyeusi.

Pamoja na mashambulizi yake yote, Ukraine ina uwezo mdogo sana wa jeshi la majini, hivyo haijaweza kutua kikosi chake kwenye kisiwa hicho.

Mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa Ukraine Oleh Zhdanov anahoji kuwa kuweka wanajeshi kwenye Kisiwa cha Snake hakuna mantiki kwa upande wowote kwani watakuwa shabaha rahisi. Badala yake, Bw Zhdanov anatetea kuunda "udhibiti wa moto" - kudumisha uwezo wa kulenga shabaha yoyote inayokaribia kisiwa hicho. 

Hilo pia lingeipa usalama mkubwa zaidi Bahari Nyeusi upande wa Ukraine hasa katika bandari ya Odesa, na sekta nzima ya kaskazini-magharibi ya Bahari Nyeusi.

Pia unaweza kusoma:

Mwamba muhimu

Urusi tayari inadhibiti sehemu kubwa ya ufuo wa Bahari Nyeusi upande wa Ukraine, pamoja na rasi ya Crimea na bahari yote ya Azov. Kushikilia Kisiwa cha Nyoka kulikuwa kumekamilisha udhibiti kamili wa mji wa bandari wa Odesa, kumaanisha usafirishaji  wa nafaka ya Ukraine nje ya nchi haungewezekana.

Ilimaanisha pia kwamba ufuo wa Bahari Nyeusi unaweza kushambuliwa pia, na wataalam wa kijeshi huko Kyiv walionyesha hofu kwamba Urusi inaweza kuweka ulinzi wa anga wa masafa marefu, kama vile mfumo wa makombora wa anga wa S-400.

Kuangalia ramani pia kunaonyesha kuwa udhibiti wa Urusi katika kisiwa hicho uliwakilisha tishio kwa mwanachama wa Nato Romania - bandari yake kuu ya Constanta na trafiki kwenye mdomo wa Mto Danube.

Sio muhimu tu kimkakati - eneo hili pia lina utajiri wa akiba ya mafuta ya petroli na gesi.

Upande wa Moscow taarifa hii

Tumezoea hili: Urusi ikitoa kauli ya matukio ambayo ni tofauti kabisa na ile iliyowasilishwa na Ukraine au nchi za Magharibi.

Moscow inataka tuamini kwamba hakukuwa na msukumo wa Warusi kutoka Kisiwa cha Nyoka.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi inadai kwamba wanajeshi wa Urusi walikuwa wamemaliza "kazi walizopewa" na kuondoka. Pia ilitaja hatua hiyo kama "ishara ya nia njema", ili kuonyesha kuwa Urusi haikutatiza usafirishaji wa chakula kutoka Ukraine.

Kwa kuzingatia umuhimu wa kimkakati wa Kisiwa cha Nyoka, ambacho kimepiganwa kwa miezi kadhaa, na kwa kuzingatia pia, ukosefu wa "ishara za nia njema" na vikosi vya jeshi la Urusi huko Ukraine tangu uvamizi huo, toleo hili la matukio litawashawishi wachache nje ya Urusi.

Kisha tena, hii inaweza kuelekezwa zaidi kwa hadhira ya nyumbani. Kremlin inataka umma wa Urusi kuamini kwamba:

Chanzo cha picha, ANDRIY YERMAK

Maelezo ya picha,

Moshi ukifuka kutoka katika Kisiwa cha Snake siku ambayo majeshi ya Urusi yaliacha eneo lenye miamba katika Bahari Nyeusi.

Kwa kuzingatia umuhimu wa kimkakati wa Kisiwa cha Nyoka, ambacho kimepiganwa kwa miezi kadhaa, na kwa kuzingatia pia, ukosefu wa "ishara za nia njema" na vikosi vya jeshi la Urusi huko Ukraine tangu uvamizi huo, toleo hili la matukio litawashawishi wachache nje ya Urusi.

Kisha tena, hii inaweza kuelekezwa zaidi kwa hadhira ya nyumbani. Kremlin inataka umma wa Urusi kuamini kwamba:

Katika mzozo huu, Warusi ni watu wazuri

Kinachojulikana kama "Operesheni Maalum ya Kijeshi" ya Kremlin nchini Ukraine inakwenda kulingana na mpango.

Kisiwa cha Nyoka kinaweza kuwa katika sehemu ya kimkakati ya Bahari Nyeusi na mahali pazuri pa kuweka mifumo ya kisasa ya makombora, lakini hatahivyo bado ni mwamba mdogo sana.

Swali kuu ni kama, kwa kuwalazimisha Warusi kutoka, Waukraine wanaweza kufikiria kuanzisha tena mauzo ya nafaka ili kuanzisha upya uchumi wao ulioharibiwa na vita.

Bila jeshi la majini lenye ufanisi, kuna uwezekano mdogo wa hilo bado, na meli za kivita za Urusi hudumisha utawala wao juu ya Bahari Nyeusi.

Ukraine imekataa ofa ya Urusi ya kusindikiza misafara ya nafaka kutoka Odessa kwani ingehitaji kuondoa migodi kutoka nje ya bandari.

Uturuki inashiriki kikamilifu katika kujaribu kujadili makubaliano na Urusi na Ukraine lakini matarajio ya hilo kutokea yanaonekana kuwa mbali katika hatua hii.

Wiki chache zijazo zinaonekana kuwa muhimu kwa mauzo ya nje ya Ukraine - kwa sababu mavuno yajayo huanza Julai.