Wanawake wanaofukiza uke kama njia ya urembo na kudumisha afya

Maelezo ya video,

Wanawake wanaofukiza uke kama njia ya urembo na kudumisha afya

Kulingana na utafiti wa Shirika la Afya Duniani WHO, nchini Msumbiji na Afrika Kusini, mwaka wa 2011, baadhi ya wanawake wanafanya mazoezi ya kufukiza uke kama njia ya kudumisha afya na utambulisho wao.

Wanawake wengine walifanya hivyo kwa muda mfupi baada ya kujifungua. Sababu zingine za kufukiza kwa uke ni pamoja na kubana uke au kama matibabu ya jumla ya urembo.

Mwanahabari wa BBC Grace Kuria ameandaa taarifa ya kufikiza uke miongoni wa wanawake vijana nchini Kenya.

Mtayarishaji:Judith Wambare