Uvutaji bangi walaumiwa kuongeza maradhi ya akili
Huwezi kusikiliza tena

Watafiti wasema mmoja kati ya wagonjwa 10 wa maradhi ya akili ni kutokana na kuvuta bangi

Kama vile mihadarati inavyosababisha madhara ya kiafya na kijamii watafiti kutoka King's College mjini London wamegundua uvutaji bangi unachangia pakubwa kuongezeka kwa maradhi ya ugonjwa wa akili hasa ule utwao. Watafiti wamegundua mmoja kati ya wa wagonjwa 10 walio na matatizo ya kisaikolijia kama ule uitwao psychosis ambapo mtu hujihisi kuwa katika mazingira tofauti ya kutatanisha akili kama vile kuwewesuka. Wagonjwa na jamii zao wanahimizwa kutafuta usaidizi wa kimatibabu ili kupunguza athari za maradhi hayo. Utafiti huu unakuja wakati baadhi ya nchi zimeondoa marufuku ya bangi kama mojawapo ya dawa za kulevya. Je nini maoni yako kuhusu uvutaji bangi? Sema nasi kwenye ukurasa wa facebook, bbcswahili.