Wakamatwa kwa kuwapiga picha za utupu wageni mahotelini
Huwezi kusikiliza tena

Wakorea kusini waghadhabishwa na wanaopiga watu picha za utupu kisiri wakiwa mahotelini

Polisi wa Korea Kusini wamewakamata watu wanne kwa kuwapiga picha wageni wapatao 1,600 katika mahoteli mbalimbali nchini humo wakiwa kwenye maeneo ya faragha kama vile vyooni na vyumbani na kisha picha hizo kuuzwa mitandaoni. Walikuwa wakitegesha vi-kamera katika maeneo mengine ambayo si ya kawaida kama kwenye TV. Walichagua picha za hasa wanawake wakiwa uchi na inasemekana walipata zaidi ya $6,200 kila mmoja walipouza picha hizo. Waliokamatwa wakipatikana na hatia wakakabiliwa na vifungo vya hadi miaka 10 na faini ya zaidi ya dolla $26,571. Jambo hilo limezua ghadhabu kubwa miongoni mwa raia wa Korea Kusini