Tangazo la 'Helmet' lililozua utata
Huwezi kusikiliza tena

Walionadi 'Helmet ya waendesha pikipiki' wakosolewa kwanini?

Tangazo hilo la kuhamasisha waendesha baiskeli kuvaa kofia ya kujikinga na ajali nchini Ujerumani imekashifiwa vikali baada ya kumuonyesha msichana aliyevaa 'helmet' akiwa tu na nguo za ndani tu -tena amelala kitandani.Mwanasiasa mmoja nchini humo amesema "picha hiyo ni aibu na uendelezaji wa mfumo dume'.Hata hivyo wizara ingali inatetea uamuzi wao wakisema unawalenga vijana. Video hiyo imeshatazamwa na watu wapatao 1.78 million. Takwimu za mwaka jana zaonesha zaidi ya waendesha pikipiki wapatao 430 walifariki kutokana na ajali za barabarani. Je unadhani kampeni hii inapitisha ujumbe mwafaka unaotakikana? Sema nasi kwenye ukurasa wa facebook, bbcswahili.