'Vifaa' vinavyotumiwa kudumaza ukuaji wa maziwa huleta madhara
'Vifaa' vinavyotumiwa kudumaza ukuaji wa maziwa huleta madhara
Baadhi ya wazazi kutoka mataifa ya Afrika wana tabia za kutumia njia zisizofaa kujaribu kuzuia mahusiano baina ya kimapenzi wavulana na wasichana ili kuepuka mimba za utotoni na mengineyo kama hayo. Njia mojawapo imefananishwa na ukatili wa ukeketaji wa wasichana ambapo wao hutumia vifaa mbalimbali kwa lengo la kukandamiza matiti ili yasikuwe wakidai huvutia wanaume kuwatongoza. Baadhi ya 'vifaa moto' vinavyotumiwa husababisha maumivu na madhara ya mda mrefu. Japo ni kinyume cha sheria inasemekana kuenezwa na hata watu wa jamii husika wanaoishi Uingereza. Idara husika wapendekeza njia mbalimbali kupambana na tamaduni hizo potovu.