Mtalii aliyefariki katika ajali ya 'Selfie' ya Nile
Huwezi kusikiliza tena

Mwili wa Msaudi aliyekufa kwa ajali ya 'Selfie' wapatikana

Mwili wa Mtalii mmoja kutoka Saudia alikufa maji baada ya kutumbukia kwenye mto Nile nchini Uganda siku ya jumamosi , sasa umepatikana.

Kwa mujibu wa polisi nchini humo, Alsubaie Mathkar alikuwa na marafiki zake katika eneo la maporomoko ya Kalagala lakini kwa bahati mbaya mahali alipokanyaga akipokuwa anajipiga picha ya Selfie palikuwa na utelezi jambo lililosababisha yeye kuteleza na kuanguka mtoni.

Imechukua juhudi nzito za vikosi vya wanamaji na wavuvi kuupata mwili wake ambao ulikuwa umesombwa na maji yaliyokuwa yakipita kwa kasi mmno.

Kumekuwa na ongezeko la ajali wakati watu wakichukua selfie katika maeneo tofauti tofauti duniani tangu kujiri kwa mitindo hiyo ya kujipiga picha kwa kutumia simu za mkononi, na baadhi ya wasimamizi wa maeneo ya kitalii wamechukua hatua za kupiga marufuku ya jumla.

Je hatua gani za kiusalama zapaswa kuzingatia unapopiga picha ye selfie?

Mada zinazohusiana