Je hatari za kuishi kwenye mikondo ya maji huzingatiwa?
Huwezi kusikiliza tena

Wakaazi wa pwani ya A. Mashariki watahatharishwa kuepuka mafuriko ya mvua inayonyesha sasa

Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, misimu ya mvua haitabiriki vyema.Huku wengi wakishuhudia mabadiliko katika maeneo waliko ambapo kwengine kumekuwa na ukame mkubwa ilhali baadhi ya maeneo yakipata mvua kupita kiasi.

Kwa sasa mvua nyingi inanyesha ukanda wa pwani ya A. Mashariki hasa Tanzania na Kenya hivyo wakaazi watahatharishwa kuepuka mafuriko. Wakaazi wa maeneo ya mabondeni na karibu na mito wamehimizwa kuhama kutokana hatari ya vifo na majeraha.

Hali hizo hukumba pia baadhi ya mataifa makubwa kama Marekani ambako kwa sasa wanaharakati za kuwahamisha wakaazi hadi maeneo salama tena kwa gharama kubwa kutokana na mafuriko ya sasa katika jimbo la Oklahoma lililokumbwa pia na kimbunga.