Burna Boy ashinda tuzo za MTV EMA
Huwezi kusikiliza tena

Mwanamuziki Burna Boy ashinda tuzo za MTV EMA

Mwanamuziki na mtunzi wa miziki wa Nigeria Burna Boy ameshinda tuzo ya muigizaji bora wa muziki barani Afrika katika tuzo za MTV EMA. Msanii huyo aliwatumbuiza wapenzi wa muziki 12,500 katika ukumbi wa Wembley mjini London. Ripoti zinadokeza kuwa ni msanii wa kwanza kutoka Afrika ambaye ameweza kutumbuiza katika ukumbi huo ukiwa umeuza tiketi zote na kujaa pomoni. Burna Boy ambaye jina lake halisi ni Damini Ebunoluwa Ogula, alianza kutia fora mwaka 2012 na kibao cha Like to Party. Albamu yake ya nne ilitoka mwezi Julai.

Ni muziki upi wa Burna Boy unaokupunga zaidi?

Tujadiliane kupitia BBCSwahili

Mada zinazohusiana