Nzige waliovamia wafukuzwa kwa kufyatuliwa risasi

Watu katika jamhuri iliyojitangazia uhuru ya Somaliland wamefyatulia risasi kundi la nzige kujaribu kuwafukuza. Maeneo mengine yaliyoathiriwa na nzige, kama vile Ethiopia , watu wamekuwa wakipiga sufuria na vifaa vingine vya kupika kujaribu kuwatishia nzige hao. Je, ni njia ipi mwafaka ya kufukuza nzige? Tueleze kwenye ukurasa wa Facebook, wa BBCSwahili.