Klopp alalamikia kuhusu mechi mbili zinazofuatana za ligi ya Premia

Klopp alalamikia kuhusu mechi mbili zinazofuatana za ligi ya Premia

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema ni ‘kosa’ kwa timu kadhaa zinazoshiriki ligi ya Premia wakitakiwa kucheza mechi mbili kwa siku tatu katika msimu wa sherehe. The reds wanatarajiwa kuelekea ugani Kings power hii leo kabla ya kuwakaribisha Wolves siku ya Jumapili. Liverpool utakuwa imecheza mechi 9 mwezi disemba pekee.