Mwaka mpya wa Uchina!
Huwezi kusikiliza tena

Mamilioni ya watu wanasherehekea mwaka mpya wa Uchina ambao ni 'Mwaka wa Panya'

Mwaka mpya wa Uchina ndiyo sherehe kubwa zaidi nchini Uchina. Pia inafahamika kama mwaka mpya wa Jadi.

Unaadhimisha kwa mara ya kwanza ambao mwezi unaandama kulingana na mzunguko wa mwezi na dunia. Mwaka huu 2020 ni mwaka wa panya unaoanza tarehe 25, Januari. Inaaminika ulianza kusherehekewa baada ya kushindwa kwa zimwi ‘Nian’ lililofukuzwa na wanakijiji waliovalia mavazi mekundu wakiwa na mataa mengi yanayong’aa na sauti kubwa za milipuko.

Chakula ni sehemu kubwa ya sherehe hizi za mwaka mpya. Baadhi ya vyakula vinathaminiwa zaidi ambavyo ni vinyunya vinavyoashiria utajiri, tambi zinaashiria maisha marefu na samaki ni taswira ya wingi. Bahasha nyekundu zinaashiria bahati nzuri. Kila mwaka hupewa jina kutokana na wanyama 12. 2020 ni mwaka wa panya mnyama anayehusishwa na werevu, busara na hekima. Mwaka wa panya ndio wa mwisho na mzungunzo unaanza upya.

Mada zinazohusiana