Huu ndio urafiki wa kweli kati ya mbwa na mwanadamu?

Huu ndio urafiki wa kweli kati ya mbwa na mwanadamu?

Mwana mitindo wa Ukraine Anastasiya Zinchenko, amekataa kuondolewa katika mji uliothirika sana na virusi vya Corona wa Wuhan baada ya kuambiwa mbwa wake Misha hangeweza kuokolewa pamoja nae. Kisa hicho kimevutia sana kimataifa,ikiwemo rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky, kumpigia simu Anastasiya kumuahidi kumrudisha Ukraine pamoja na mbwa wake.