Wanawake 48 watolewa vizazi bila idhini zao

Mwanamke mmoja nchini Afrika Kusini ameiambia BBC jinsi alivyotolewa kizazi bila idhini yake baada ya kujifungua akiwa na umri wa miaka 17 ,na kujua kuhusu tukio hilo miaka 11 baadaye wakati alipojaribu kupata mtoto mwingine. Bongekile Msibi ni kati ya wanawake 48 waliotolewa vizazi bila idhini zao katika hospitali za serikali. Haya yamefichuliwa na tume ya usawa na jinsia.