Ndege wanisaidia kukabiliana na ugonjwa wa kiakili

Ndege wanisaidia kukabiliana na ugonjwa wa kiakili

Mwanamke mmoja amefurahishwa na hatua ya mamia ya watu kujibu mwaliko alioufanya kupitia ukurasa wa Facebook kukutana naye pamoja na kundi lake la ndege walio nadra. Rachel Pickett-Nunn kutoka Lowestoft, Suffolk, amesema ndege hao wameokoa maisha yake baada ya ugonjwa wa akili kumuathiri sana kwa sababu ya ulemavu.