Matamshi ya Muigizaji Vanessa Hudgens kuhusu Corona yakera wengi

Muigizaji wa filamu ya muziki ya The High School Musical,Vanessa Hudgens ameomba msamaha baada ya kukososlewa vikali alipoweka video kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema kila mtu atakufa hata kukiwa hakuna virusi vya Corona. Mjadala uliopo mitandaoni kwa sasa ni kuwa watu wengi mashuhuri hawana uelewa kamili wa virusi hivi.