Kasisi afariki na maambukizi ya corona

Kasisi wa kiitaliano aliyegawa kifaa chake cha kumsaidia kupumua kwa mgonjwa wa corona aliyekuwa na umri mdogo amefariki kutokana na ugonjwa huo.

Inasemekana kuwa Padre Giuseppe Berardelli, alikataa kutumia kifaa alichonunuliwa na waumini wa kanisa lake na kumpa mgonjwa mwenye corona.