Bei ya Juisi ya machungwa imepanda kwa aslimia 20

Bei juisi ya machungwa imekadiriwa kupanda kwa zaidi ya 20% mwezi huu kwani watu wanatafuta bidhaa zenye afya wakati huu wa janga la coronavirus.

Huku hitaji la machungwa likiongezeka, ugavi wa bidhaa hii umepungua huku wazalishaji waking’ang’ana kusafirisha bidhaa kutokana na vizuizi vya usafirishaji vilivyowekwa kufwatia janga la Korona.

Je, vipi bei ya bidhaa hii katika eneo lako? sema nasi kwenye ukurasa wa Facebook, wa BBCSwahili.