Kuzuia maambukizi ya Covid 19 ni hatia kutembesha mbwa Afrika Kusini

Waziri wa usalama nchini Afrika Kusini Bheki Cele ametangaza mabadiliko ya uamuzi wa kuwaruhusu wamiliki wa mbwa kutembea na wanyama wao wakati wa kizuizi cha siku 21 kinachoanza kutumika Ijumaa ili kukabiliana maambulizi ya virusi vya corona. Waziri wa afya Zweli Mkhize awali Jumatano alisema kuwa watu wangeruhusiwa kukimbia na kutembea na mbwa wao, mradi wangefanya kwa uwajibikaji.