Wavutaji sigara Afrika Kusini wahangaika kufwatia marufuku.

Wavutaji sigara Afrika Kusini wahangaika kufwatia marufuku.

Biashara haramu ya sigara nchini Afrika Kusini inaendelea kufanyika licha ya kupigwa marufuku mwisho wa Machi kama sehemu ya hatua zilizowekwa kupunguza kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Corona. Sheria hizo za Afrika Kusini ni kati ya kali zaidi ulimwenguni zikiwa ni pamoja na kupiga marufuku uuzaji wa pombe.