Baiskeli zatumiwa kama ‘daladala’ Shinyanga, Tanzania

Baiskeli zatumiwa kama ‘daladala’ Shinyanga, Tanzania

Baiskeli hutumika kama chombo cha usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, hali ni tofauti mkoani Shinyanga, kaskazini magharibi mwa Tanzania, ambapo baiskeli zinajulikana kama daladala, kutokana na kutumika kibiashara kwa kufanya kazi ya kusafirisha abiria.

Mwandishi wa BBC Esther Namuhisa alizuru Shinyanga hivi karibuni na kutumia usafiri huo wa kipekee daladala.