Wafanyakazi wa China washambuliwa Kenya

Ujenzi wa Reli

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ujenzi wa reli

Kundi moja la vijana waliojawa na ghadhabu na ambao walikuwa wamejihami na fimbo waliwavamia raia wa Uchina wanaofanya kazi ya ujenzi wa barabara ya kisasa ya Treni nchini Kenya.

Wafanyikazi 14 wa China walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo katika eneo la Narok, takriban kikomita 200 kusini magharibi mwa mji wa Nairobi.

Washambuliaji hao walidaiwa kulalamikia kampuni ya kujenga barabara na madaraja ya China kwa kutowapatia ajira za ujenzi wa reli hiyo.

Makumi ya maafisa wa polisi wamepelekwa katika eneo hilo huku mamlaka ikifanya mikutano ya dharura kwa lengo la kutuliza hali.

Kuna Takriban raia 4000 wa China wanaofanya kazi nchini Kenya hususan katika viwanda vya ujenzi pamoja na biashara za kuuza vifaa vya kielektroniki.