Visa vya utumikishwaji wa watoto Tanzania vyashuka

Visa vya utumikishwaji wa watoto Tanzania vyashuka

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni kuhusu utumikishwaji wa watoto nchini Tanzania inaonyesha asilimia 28 ya watoto wote wa nchi hiyo wanatumikishwa katika kazi ngumu na za hatari.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo watoto hao wamekuwa wakitumikishwa katika maeneo hatarishi kama vile kwenye migodi ya madini, kilimo, misitu na uvuvi.

Hata hivyo ripoti hiyo inaonyesha kupungua kidogo kwa tatizo hilo ikilinganishwa na miaka kumi iliyopita ambapo watoto waliokuwa wakitumikishwa walikuwa ni asilimia 30 ya watoto wote.

Mwandisihi wetu Tulanana Bohela anatuarifu zaidi.