Madereva wa Uber wameandamana kupinga punguzo la bei

Madereva wa Uber wameandamana kupinga punguzo la bei

Siku chache tu baada ya kampuni inayoendesha huduma ya teksi ya Uber kutangaza punguzo la bei ya huduma hiyo ya usafiri, wahudumu na wamiliki wa teksi zinazotumia huduma hiyo mjini Nairobi Kenya wameandamana wakidai punguzo hilo linawapunguzia mapato na hivyo kuhatarisha kitega uchumi chao.

Uber ilitangaza punguzo la asilimia 35% ya bei ya usafiri ilikuimarisha ushindani wake dhidi ya kampuni zingine zinazotoa huduma ya teksi.