Mahakama kujadili mapenzi ya jinsia moja Indonesia

Mapenzi ya Jinsia moja nchini Indonesia
Maelezo ya picha,

Mapenzi ya Jinsia moja nchini Indonesia

Mahakama ya kikatiba ya Indonesia inajadili iwapo mapenzi ya jinsia moja yanafaa kuwa uhalifu.

Mahakama hiyo ya juu ilikubali ombi lililowasilishwa na kundi moja la wanaharakati wa Kiislamu Family Love Alliance.

Mapenzi ya jinsia moja ni halali katika maeneo mengi ya Indonesia ,lakini wapenzi wa jinsia moja wamekuwa wakibaguliwa katika kipindi cha mwaka mmoja baada ya viongozi kadhaa wa kidini kuikana jamii hiyo.

Mtandao wa mahakama hiyo unasema kuwa utasikiliza ushahidi kutoka kwa maafisa wa afya ambao wanaamini kwamba mapenzi ya jinsia moja yanaweza kueneza magonjwa ya zinaa,lakini wakosoaji wanasema kuwa hayo hutokea hata miongoni mwa wasioshiriki katika mapenzi hayo.