Upishi wa kisasa wa pweza wavuma Dar
Huwezi kusikiliza tena

Upishi wa kisasa wa pweza wavuma Dar

Samaki aina ya Pweza wanaovuliwa ndani ya Bahari ya Hindi ni maarufu katika maeneo mengi ya Pwani ya Afrika Mashariki.Jijini Dar es Salaam kila upitapo katika maeneo mengi ni nadra kukosa kuona makundi makundi ya watu wakiwa wamezunguka meza katika ukingo wa barabara,wakila finyango za pweza.

Lakini kwa sasa maandalizi ya pweza yemebadilika na kuandaliwa kisasa zaidi na kufikia hatua ya kuliwa katika migahawa tofauti na zamani.

Mwandishi wa BBC Esther Namuhisa amefuatilia zaidi mfumo mpya wa maandalizi ya samaki huyo.