Wakonta Kapunda, msichana anayeandika kwa ulimi

Wakonta Kapunda, msichana anayeandika kwa ulimi

Kutana na Wakonta Kapunda, msichana wa miaka 25 kutoka Tanzania ambaye alipata ajali siku ya kuhitimu sekondari.

Baada ya matibabu na kulazwa hospitalini kwa miezi, miaka minne baadaye amepooza mwili mzima isipokuwa shingoni na kichwani.

Lakini sasa amepata matumaini baada ya kujifundisha namna ya kuendeleleza ndoto yake ya uandishi wa filamu kutumia ulimi wake, ambao ndio pia anaotumia kujibia simu na kuandika ujumbe mfupi wa simu ya mkononi.

BBC ilikutana naye katika mashindano ya uandishi aliyoshiriki kisiwani Zanzibar.