Bintiye Obama afanya kazi mgahawani

Sasha Obama, 15, akifanya kazi

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha,

Sasha Obama, 15, akifanya kazi

Sasha Obama, bintiye Rais wa Marekani Barack Obama, ameamua kuacha 'starehe' za ikulu ya White House na kuanza kufanya kazi katika mgahawa mmoja, vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.

Binti huyo wa umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha's Vineyard, Massachusetts.

Sasha, ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliandamana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.

Familia ya Obama hutembelea eneo hilo sana wakati wa likizo.

Picha zinazosambazwa zinamuonesha bintiye huyo mdogo wa Obama akiwa amevalia sare ya hoteli akifanya kazi.

Mfanyakazi mmoja katika mgahawa huo aliambia gazeti hilo la Herald: "Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na watu sita walikuwa wanamsaidia msichana huyu, lakini baadaye tukagundua alikuwa nani."