Watu 13 wafariki katika baa Ufaransa

Baa nchini Ufaransa Haki miliki ya picha Jakob Hoff
Image caption Baa nchini Ufaransa

Takriban watu 13 wameaga dunia kwenye ajali ya moto kwenye baa katika mji wa Rouen kaskazini mwa ufaransa.

Watu wengine sita walijeruhiwa wakati wa ajali hiyo ambayo ilitokea wakati wa sherehe za kuzaliwa.

Waziri wa mambo ya ndani Bernard Casseneuve alisema kuwa wazima moto 50 walifika eneo hilo

Uchunguzi umeanzishwa.

Mada zinazohusiana