Hiroshima waadhimisha miaka 71 tangu ushambuliwe
Maelfu ya watu katika mji wa Hiroshima nchini Japan amehudhuria sherehe za kila mwaka kuadhimisha kaharibiwa kwa mji huo miaka 71 iliyopita wakati wa shambulizi la kwanza la bomu la nuklia.

Hiroshima
Manusura ambao kwa sasa ni wazee walijiunga na watu wengine kusikia kengele ya amani eneo ambapo bomu la atomic la marekani lililipuka na kuwuaa takriban watu 140,000
Waziri mkuu wa Japana Shinzo Abe ameahidi kujitolea kuhakisha kutokuwepo ulimwengu wenye silaha za nuklia.
Waziri mkuu wa Japan Sinzo Abe
Alipongeza matamshi ya rais wa marekani Barack Obama ambaye mapema mwaka huu alikuwa rais wa kwanza wa marekani kuzuru mji wa Hiroshima.