Moto waua watu 13 nchini Ufaransa

wazimoto wakabiliana na moto huo Haki miliki ya picha AFP
Image caption wazimoto wakabiliana na moto huo

Moto uliozuka kwenye kilabu kimoja katika mji ulio kaskazini mwa Ufaransa wa Rousen wakati wa sherehe ya siku ya kuzaliwa ulisababisha vifo vya karibu watu 13 na kuwajeruhi wengine sita.

Mishumaa kwenye keki ndiyo ilianzisha moto huo katika klabu ya Cuba Libre, ambao ulianza saa sita usiku ,siku ya Jumamosi.

Dari la chumba ambacho kilishika ilikuwa imetengenezwa kwa plastiki,kulingana na shirika la habari la AFP

Waziri wa mambo ya ndani Bernard Cazeneuve, amesema zaidi ya wazima moto 50 waliitwa kuuzima moto huo.

Kwa hivi sasa uchunguzi unaendelea.

Mtu mmoja kati ya waliojeruhiwa yuko katika hali mahututi

Swala la ujambazi limetupiliwa mbali.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mishumaa ya keki ilisababisha moto
Haki miliki ya picha AP
Image caption Chupa zilizoharibiwa na moto

Mada zinazohusiana