Manchester City wamsajili mshambuliaji mpya

Image caption Marlos Moreno

Manchester City wamemsajili mshambulizi Marlos Moreno kwa kitita cha pauni milioni 4 kwa muda wa miaka mitano kutoka Atletico Nacional ya Colombia.

Moreno mwenye umri wa miaka 19, atajiunga kwa mkopo na klabu ya Uhispania ya Deportivo La Coruna msimu wa 2016-17.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pep Guardiola

Mshambuliaji huyo atakuwa mchezaji wa tatu kwa meneja Pep Guardiola kumsajili wiki hii, baada ya kumchukua winga Leroy Sane kutoka Schalke na mshambuliaji Gabriel Jesus kutoka Palmeiras.

Tangu kuondoka kwa Maneuel Pellegrini mwezi wa Julai, Guardiola ametumia zaidi ya pauni milioni 100 kwa matumizi ya klabu hiyo.

Moreno ameandika kwenye tovuti ya klabu hiyo kwamba Pep Guadiola ni 'meneja bora zaidi ulimwenguni'.