Bauza kumshawishi Messi arejee kikosini

Lionel Messi akiichezea Argentina

Chanzo cha picha, Mike Stobe

Maelezo ya picha,

Lionel Messi ameichezea Argentina mechi 113 tangu 2005

Kocha mpya wa Argentina Edgardo Bauza ameapa kumshawishi mshambulizi wa Barcelona kurejea uwanjani kuipeperusha bendera ya Argentina baada ya kutangaza kuwa amestaafu alipokosa mkwaju wa penalti katika mchuano wa Copa Merica.

Mshambulizi wa klabu ya Uhispania Barcelona Messi astaafu mwenye umri wa miaka 29 alitangaza kustaafu soka ya kimataifa mwezi Juni punde baada ya kukosa mkwaju wa penalti dhidi ya Chile katika mchuano wa kuwania kombe la Copa Merica.

Hiyo ilikuwa kichapo chao cha nne katika fainali ya michuano ya kimataifa katika kipindi cha miaka 9.

Bauza aliyerithi nafasi iliyoachwa wazi na Gerardo Martino amenukuliwa akisema kuwa nia yake ni kukutana na Messi na kisha kumshawishi arejee uwanjani.

''Bila shaka baada ya mazungumzo nitatafakari iwapo ataitwa katika kikosi cha taifa kwani bado tunamechi ngumu tunazomhitaji''

Argentina wameratibiwa kuchuana dhidi ya Uruguay na Venezuela katika juma la kwanza la Septemba katika mechi za kuwania kombe la dunia la mwaka wa 2018.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Kocha mpya wa Argentina Edgardo Bauza ameapa kumshawishi mshambulizi wa Barcelona kurejea uwanjani

Argentina wanashikilia nafasi ya 3 nyuma ya vinara uruguay na Ecuador.

Washindi wa kwanza wanne wanajikatia tikiti ya moja kwa moja huku timu inayorodheshwa ya tano ikishiriki michezo ya maondoano.

Bauza, 58, ni mshambulizi wa zamani wa klabu ya Copa Libertadores ambaye ameiongoza klabu hiyo hiyo katika michuano mbili ya kuwania ubingwa wa kusini mwa Marekani.