Kenya yakabiliwa na madai mapya

Chanzo cha picha, PA
Kenya imepata shinikizo kubwa kupambana na madawa hayo haramu
Huku mashindano ya Olimpiki yakiendelea huko Rio nchini Brazil, mamlaka kuu ya kuchunguzi matumizi ya dawa za kusisimua misuli nchini Kenya, inasema itachunguza madai mapya dhidi ya meneja mkuu wa kikosi cha wanariadha wa nchi hiyo.
Gazeti la Sunday Times la jijini London, limetoa ukanda mpya wa video unayoonyesha Meja Michael Rotich, akiwaonya wanariadha wa kikosi chake ya kuzuru mamlaka kuu ya kupima matumizi ya dawa hizo, wakiwa tayari kutoa mlungula wa pauni elfu kumi £10,000.
Meja Rotich ni meneja mkuu wa kikosi cha wanariadha wa Kenya.
Ilani ya mapema anasema itawapa wanariadha muda wa kusafisha chembechembe za dawa hizo kutoka mwilini mwao.
Meja Rotich anaripotiwa kukanusha kuwa hajafanya lolote baya, huku akiongeza kuwa alizungumza na maripota hao wa kujificha, ili kutaka kuwafahamu ni akina nani hasa na nini walichokuwa wakikitafuta.
Gazeti hilo la Sunday Times na runinga ya Ujerumani ARD lilimrekodi afisa huyo bila yeye kujua kuwa alikuwa akirekodiwa.
Chanzo cha picha, AFP
Kenya yakabiliwa na madai mapya ya utumizi wa madawa
Mkurugenzi wa shirika la kupambana na madawa ya kuongeza nguvu mwilini ADAK Japhter Rugut ameahidi kuchunguza madai hayo kikamilifu.
Madai hayo yanatokea siku mbili tu baada ya shirika la kupambana na madawa duniani WADA kuiondoa Kenya kwenye orodha ya mataifa ambayo yanakiuka kanuni za vita dhidi ya udanganyifu michezoni na utumizi wa madawa ya kusisimua misuli.
Kenya ilikuwa imewekwa kwenye orodha hiyo baada ya kushindwa mara mbili kutekeleza matakwa makali ya shirikisho la dunia la WADA.