Oscar Pistorius ajeruhiwa gerezani

Oscar Pistorius Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Oscar Pistorius

Maafisa wa magereza nchini Afrika Kusini, wanasema kuwa mwanariadha mlemavu wa nchi hiyo Oscar Pistorius, ametibiwa hospitalini baada ya kupata majeraha akiwa korokoroni.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake

Msemaji wa idara ya magereza nchini humo, amesema kuwa Pistorius alianguka kutoka juu ya kitanda chake, lakini kwa sasa amerejeshwa gerezani anakohudumia kifungo cha miaka sita kwa kosa la kumuuwa mpenziwe wa kike Reeva Steenkamp.

Kuna ripoti inayosema kuwa alikuwa amejeruhiwa kwenye kifundo cha mkono.

Kumeibuku uvumi katika mitandao ya kijamii nchini Afrika Kusini kuwa Pistorius alikuwa amejaribu kujitia kitanzi lakini hilo limekanushwa na familia ya mwanariadha huyo.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Reeva Steenkamp

Mwezi uliopita, waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini, walisema kuwa watakata rufaa kupinga hukumu ya miaka sita ya Pistorius, wakisema kuwa ni hukumu ndogo mno.

Mwanariadha huyo alimuuwa mpenziwe wa kike , kwa kumpiga risasi nyumbani kwake wakati wa siku kuu ya wapendanao mnamo mwaka wa 2013, akisema kuwa alidhania ni mwizi.