Zoezi latangulia mkutano wa baraza la mawaziri

Rais mpya wa Peru Pedro Pablo Kuczynski aliwaacha wengi vinywa wazi kwa kufanya mazoezi hadharani na mawaziri kabla ya kikao cha kwanza cha baraza la mawaziri katika mji mkuu wa Lima.

Picha ya baraza la mawaziri la Peru Agosti 4, 2016

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais na mawaziri wafanya zoezi hadharani

Rais Kuczynski (kulia), mwenye umri wa miaka 77, alionekana akijifua sambamba na muziki wa kasi wa kisasa unaotumika kuwatia shime watu wafanye zaozi.

Baraza la mawaziri lilikuwa linajiandaa kwa mkutano muhimu kabla ya rais huyo kuwajulisha kuwa ilikuwa vyema wafanye wote mazoezi katika bustani ya ikulu.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rais Pedro Pablo Kuczynski akiliongoza zoezi la baraza la mawaziri

"tungependa kuchochea baraza la mawaziri liwe na afya njema kwani wakiwa katika hali njema ya siha ni rahisi wao kuwahudumia wananchi kwa shime'' alisema bwana Mr Kuczynski .

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Baraza la mawaziri likifanya zoezi Peru

Waziri wa afya bi Patricia Garcia alisema kuwa baraza la mawaziri na rais watakuwa wakijifua kila wiki kama njia ya kuwachochea raia wa taifa hilo kuiga mfano na kukomesha unene wa kupita kiasi ambao unaonekana kukithiri katika miji mingi nchini humo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Rais Pedro Pablo Kuczynski akikimbia

Hata hivyo zoezi hilo la baraza la mawaziri halikuhudhuriwa na mawaziri wawili : waziri wa elimu , Jaime Saavedra, aliyewasili akiwa amevalia suti.

Alisikika akiwaambia waandishi wa habari kuwa atawashawishi wanafunzi na walimu kutilia mkazo swala la afya ya wasomi na haswa mazoezi kama hayo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Kila mjumbe alijiandaa kabla ya mazoezi hayo kuanza

Mwengine ambaye alikosa zoezi hilo rasmi alikuwa waziri wa kilimo Jose Manuel Hernandez Calderon, ambaye amejeruhiwa na hivyo asingeweza kujifua na rais na wenzake.