Thailand kuruhusu jeshi kuendelea kutawala

Wapiga kura nchini Thailand wameidhinisha katiba mpya ambayo itaruhusu jeshi kuendelea kuongoza taifa ilo.

Image caption Raia wa Thailand wakipiga kura

Kampeni zote za kupinga uamuzi huo zikiwa zimezuiliwa na serikali ya kijeshi pasipo kutoa ufafanuzi wa kutosha.

Matokeo ya kura zilizopigwa yanaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura wanaunga mkono mabadiliko ya katiba. Huku asilimia hiyohiyo ndiyo itakayohusika kumchagua waziri mkuu.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nchi ya Thailand inaongozwa kijeshi baada ya kufanya mapinduzi miaka miwili iliyopita.

Nchi ya Thailand inaongozwa kijeshi baada ya kufanya mapinduzi miaka miwili iliyopita. Jeshi linaamini kuwa katiba mpya itaimarisha nchi hiyo kufuatia misukosuko ya kisiasa iliodumu kwa takribani miaka kumi.

Kuhusu BBC