Visiwa vya Sao Tome kurudia uchaguzi mkuu

Visiwa vya Sao Tome na Principe moja kati ya nchi ndogo zaidi barani Afrika, imeaingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Rais Rais aliye madarakani Manuel Pinto Da Costa amewataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo.

Image caption Rais Manuel Pinto Da Costa (kushoto) amekua wa pili katika duru ya kwanza ya uchaguzi

Rais Manuel Pinto Da Costa amekua wa pili katika duru ya kwanza ya uchaguzi . amesema uchaguzi huo haukua wa haki na amewataka wafuasi wake wasishiriki katika duru ya pili huku mgombea mwenza, spika wa zamani wa bunge anaonekana kushinda. Pinto Da Costa amekua rais tangu mwaka 2011 ameiongoza nchi hiyo kwa kipindi cha chama kimoja kutoka kupata kwake uhuru mwaka 1975 hadi 1991.