Urusi yafungiwa kushiriki Paralympic mwezi ujao

Kamati ya kimataifa ya Paralympic imeifungia Urusi kushiriki michezo ya mwezi ujao mjini Rio, Brazil kwasababu ya wanamichezo wake wamehusika katika ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli.

Rais wa kamati hiyo Philip Craven amesema Urusi imekuwa na mifumo mibovu na iliyojaa rushwa jambo ambalo ni kinyume na taratibu za mashindano hayo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rio itakuwa mwenyeji wa michezo ya Paralympic mwezi ujao

Waziri wa michezo wa Urusi Vitaly Mutko, amesema uamuzi huo sio sahihi na nchi yake itakata rufaa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Goncharova wa Urusi ameshinda medani tatu za dhahabu Paralympic

Mwezi ulipita kamati ya Olimpiki ilikoselewa vikali baada ya kushindwa kuifungia Russia kushiriki mashindano hayo.