Tamasha la Afrika Mashariki lafanyika jijini Dar es Salaam
Huwezi kusikiliza tena

Tamasha la muziki la Afrika Mashariki lafanyika Dar es salaam

Tamasha la The East Africa Vibes Concert limerejea jijini Dar es Salaam mwisho wa wiki hii huku mashabiki wengi waliohudhuria wameeleza kukongwa nyoyo sana na burudani iliyotolewa. Mwaka huu likiwa limebeba maudhui ya Vukaboda, tamasha hili linalenga kuibua na kuinua vipaji vya wanamuziki na washairi katika jitihada za kujenga wanamuziki makini katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Mwandishi wetu Sammy Awami alihudhuria pia tamasha hilo na akatuandalia taarifa ifuatayo.