Kwa Picha: Watoto waliodumaa India

WaterAid/Ronny Sen

Chanzo cha picha, WaterAid/Ronny Sen

Maelezo ya picha,

Ripoti ya WaterAid inaonesha India ina watoto 48 milioni waliodumaa

India ina kiwango cha juu zaidi cha watoto waliodumaa duniani, shirika la misaada la WaterAid limesema katika ripoti mpya.

Ripoti hiyo kwa jina Caught Short, inasema India ina watoto takriban 48 milioni nchini humo ambao wana umri wa chini ya miaka mitano, wamedumaa.

Nigeria na Pakistan zinafuata katika nafasi ya pili na tatu mtawalia, zikiwa na watoto 10.3 na 9.8 milioni mtawalia.

Kuduma kwa watoto hutokana na ukosefu wa lishe bora miaka miwili ya kwanza ya mtoto, kwa kiasi kikubwa huwa madhara yake hudumu. Kuduma kwa watoto pia huathiri ukuaji wa watoto kiakili.

Chanzo cha picha, WaterAid/Ronny Sen

Kando na ukosefu wa chakula, matatizo mengine kwa mfano uchafu na ukosefu wa maji safi ya kunywa pia husababisha utapiamlo na kuchangia kudumaa kwa watoto.

Chanzo cha picha, WaterAid/RonnySen

Robo ya visa vyote vya kudumaa vinaweza kuhusishwa moja kwa moja na kuugua ugonjwa wa kuharisha miaka miwili ya kwanza ya mtoto.

Chanzo cha picha, WaterAid/Ronny Sen

Takriban watu 76 milioni huwa hawana maji safi ya kunywa India.

Chanzo cha picha, WaterAid/Ronny Sen

...na 774 milioni huishi bila vyoo na huduma nyingine za usafi. Watoto 140,000 hufariki kila mwaka kutokana na kuharisha India.

Chanzo cha picha, WaterAid/Ronny Sen

Watu kwenda haja kubwa maeneo wazi ni tatizo kubwa sana la kiafya India.

Chanzo cha picha, WaterAid/Ronny Sen

Miaka ya karibuni, India imepiga hatua katika kupunguza visa vya watoto kudumaa. Karibu watoto 48% nchini India waligunduliwa kuwa wamedumaa mwaka 2006, lakini visa hivyo vilishuka hadi 39% mwaka 2014, shirika la WaterAid linasema.

Waziri Mkuu Narendra Modi amelipa kipaumbele suala la kutoa maji safi na huduma za usafi kwa raia wote India katika serikali yake.