Waandamanaji 100 waliuawa Ethiopia- Amnesty

Image caption Waethiopia wazika waliouawa katika maandamano

Waethiopia '100 waliuawa' kufuatia machafuko yaliyotokea wikiendi iliyopita polisi walipokabiliana na waandamanaji wa Oromia na Amharia shirika la kutetea haki za kibinadamu lenye makao yake nchini Marekani Amnesty International linasema.

Zaidi ya watu 30 waliuawa katika jimbo lililoko Kaskazini Magharibi la Bahir Dar siku ya Jumapili.

Serikali hata hivyo imekuwa ikishikilia kuwa ni watu 7 pekee waliouawa katika makabiliano mabaya zaidi kati ya wenyeji na maafisa wa usalama.

Awali Waethiopia waliwazika wahanga wa makabiliano makali baina ya waandamanaji na maafisa wa polisi katika mji wa kaskazini magharibi mwa Bahir Dar.

Maafisa wa utawala katika mji huo wanasema kuwa takriban watu 7 walipoteza maisha yao katika maandamano hayo yaliyochacha mwishoni mwa juma.

Jumapili ilishuhudia makabiliano makali baina ya waandamanaji na maafisa wa utawala.

Waandamanaji hao walikuwa wakipinga sera mpya ya serikali ya kupanua jiji la Addis Ababa ambayo ililazimu baadhi yao kupokonywa ardhi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Maelfu ya watu waliandamana dhidi ya sera ya serikali kuwapokonya ardhi

Waandamanaji walifunga mabarabara na kuimba nyimbo zinazopinga utawala ulioko sasa Ethiopia.

Wapiganiaji haki za kibinadamu wanasema kuwa idadi ya wale waliouawa katika siku tatu za maandamanao ni juu zaidi ya saba waliotajwa na maafisa wa serikali.

Miili ya vijana wawili ilizikwa leo katika eneo la hilo.

Image caption Ramani ya Ethiopia

Inaaminika kuwa wawili hao waliuawa na maafisa wa utawala.

Kulishuhudiwa pia maandamano makubwa katika eneo la Oromia ambako kunaaminika kuwa watu kadhaa waliuawa.

Hata hivyo idadi kamili haijulikani.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii