Shirika la ndege Marekani Delta lasitisha safari zake

Shirika la ndege Marekani, la Delta, limetangaza kusitisha na kuchelewesha safari zake baada ya kutokea matatizo ya mfumo wa komputa wa ndege zake kote duniani.

Delta imesitisha tena safari baada ya kukatisha safari zake siku ya jumatatu na kuwaacha maelfu ya wasafiri wakihangaika.

Image caption Baadhi ya abiria waliokwama

kushindwa kwa mfumo wa komputa wa kampuni hiyo ulisababishwa na kukatika kwa umeme katika makao mkuu mjini Atlanta.

Image caption Delta imesitisha tena safari baada ya kukatisha safari zake siku ya jumatatu

Shirika hilo la Delta limesema kuwa abiria waliositishiwa safari au kucheleweshwa watapewa ndege nyingine au kurudishiwa gharama zao.