Muhtasari: Habari kuu leo Jumanne

Miongoni mwa habari nyingine kuu leo, Trump ameanza kuangazia uchumi katika kampeni yake, Marekani imesikitishwa na mauaji ya walanguzi wa dawa Ufilipino.

1. Trump aanza kujikita katika uchumi

Haki miliki ya picha Getty Images

Mgombea wa urais kwa tiketi ya chama cha Republican Donald Trump amebadilisha mwelekeo wa kampeni yake hadi maswala ya kiuchumi baada ya wiki ya migogoro.

Akizungumza huko Detroit, ameahidi kuuchapua uchumi wa Marekani kupitia kuondoa kanuni mpya na kupunguza kodi kwa mashirika.

2. Ugomvi mwingine wazuka kuhusu Trump Republican

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aliyekuwa mkuu wa CIA Michael Hayden

Wakati huo huo ugomvi umezuka kati ya Donald Trump na maafisa 50 wa usalama waliohudumu katika utawala wa rais wa zamani George Bush.

Maafisa hao walitoa taarifa wakisema kuwa Trump atakuwa rais asiyejali katika historia ya taifa hilo.

3. Marekani yasikitishwa na mauaji Ufilipino

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Rodrigo Duterte amesema hatawavumilia walanguzi wa dawa za kulevya

Marekani imeeleza wasiwasi wake kuhusu ripoti kutoka Ufilipino kuhusu mauaji ya kiholela dhidi ya washukiwa wa dawa za kulevya yanayotekelezwa na polisi.

Polisi nchini Ufilipino wanasema kuwa wamewaua washukiwa 400 wa ulanguzi wa mihadarati katika kipindi cha miezi mitatu.

4. Jeshi Mexico laendelea na juhudi za uokoaji

Haki miliki ya picha AP

Wanajeshi wa Mexico na waokoaji wanatafuta watu waliotoweka kufuatia kimbunga Earl, ambacho kimesababisha maporomoko na kuwaua takriban watu wanne tangu Jumamosi.

Nyumba nyingi zilizikwa na matope katika jimbo la mashariki la Veracruz na eneo jirani la Puebla.

5. Chanzo cha kupungua kwa samaki Tanganyika

Haki miliki ya picha Getty Images

Utafiti mpya unasema kuwa kupanda kwa viwango vya joto katika kipindi cha karne moja iliopita ndio sababu ya kupungua kwa viwango vya samaki katika ziwa Tanganyika.

Ziwa hilo ni chanzo muhimu cha chakula miongoni mwa mamilioni ya raia wa Afrika Mashariki.

6. Brazil yashinda medali ya kwanza Brazil

Haki miliki ya picha BBC Sport

Brazil inasheherekea medali ya kwanza ya dhahabu katika michezo ya olimpiki ya Rio. Rafaela Silva alishinda katika mchezo wa judo uzani wa kilo 57.

Medali hiyo ya dhahabu inaonekana kuwa ufanisi mkubwa kwa mwanariadha aliyekulia katika mtaa maskini na wenye sifa mbaya zaidi.

7. Manchester United wamsajili Pogba

Haki miliki ya picha Getty Images

Na hatimaye klabu ya Manchester United imemsajili kiungo wa kati raia wa Ufaransa, Paul Pogba katika uhamisho unaodaiwa kuwa ghali zaidi.

Pogba amejiunga na klabu hiyo ya Uingereza kwa kitita cha dola milioni 150 kutoka Juventus.