Uhusiano baina ya Uingereza na Uchina mashakani

Hinkley Point
Image caption Hinkley Point

Uchina imeonya kwamba huenda uhusiano wake wa siku zijazo na Uingereza ukatatizika ikiwa mradi wa mabilioni ya dola wa ujenzi wa mtambo wa nyuklia hautaendelea.

Uchina inatarajia kudhamini theluthi moja ya ujenzi uliopangwa wa kiwanda cha nyuklia wa Hinkley Point kusini mwa Uingereza.

Lakini mwezi uliopita serikali ya Uingereza ilitangaza kuutathmini upya mradi huo kufuatia hofu iliyopo ya hali ya usalama kuhusu kuhusishwa kwa Uchina.

Katika taarifa aliyoitoa kwenye gazeti la Financial Times, balozi wa Uchina mjini London Liu Xiaoming ameitaka serikali ya Uingereza kufanya uamuzi wa mwisho haraka .

Amesema kuwa uhusiano baina ya Uingereza na Uchina uko njia panda.