Mpinzani mpya wa Donald Trump, Evan Macmullin ni nani?

Evan McMullin: Afisa wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA
Image caption Evan McMullin: Afisa wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA

Afisa wa zamani wa CIA Evan McMullin amezindua kampeni huru ya kuwania urais wa marekani akiungwa mkono na wanachama wa vuguvugu linalopinga Donald Trump maarufu kama Never Trump

McMullin, anatarajiwa kujiandikisha rasmi kama mgombea wa urais Jumatatu.

Huenda akakumbwa na changamoto za kutimiza tarehe ya mwisho ya kura na pia kutafuta ufadhili miezi mitatu kabla ya siku ya kura.

McMullin mwenye umri wa miaka arobaini, hajawahi kuwa kiongozi katika nyanja za kisiasa.

McMullin ambaye si maarufu sana na hana mke, ni mhadhifina aliyewahi kufanya kazi na Shirika la Ujasusi CIA kwa miaka 11 hadi mwaka wa 2010.

Haki miliki ya picha Getty Images

Baadaye alijiunga na kamati ya mambo ya nje kama mshauri mwandamizi wa usalama wa taifa mwaka wa 2013

Mzaliwa wa Utah, alihitimu katika chuo kikuu cha Brigham Young na shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara.

Kwenye akaunti yake ya Twitter alikuwa na wafuasi 135 pekee kabla ya kutangaza azma yake ya kuwania Urais, alipata wafuasi zaidi ya 12000 masaa machache baada ya kutangaza.

McMullin ametangaza wazi kumpinga Donald Trump katika mitandao ya kijamii akimuita Trump kama kiongozi wa Kimabavu na pia kukashifu vikali matanmshi ya Trump kuhusu familia ya mkongwe wa vita Humayan Khan