Wasukuma na utamaduni wa kutakasa mapacha
Huwezi kusikiliza tena

Wasukuma na utamaduni wa kutakasa mapacha

Katika miaka ya hivi karibuni, uzazi wa watoto mapacha umeonekana kuvutia wengi huku baadhi ya wanandoa wakijaribu kutumia njia za kisasa kuhakikisha wanazaa mapacha.

Lakini miongoni mwa jamii ya wasukuma huko kaskazini magharibi mwa Tanzania,uzazi wa watoto mapacha unaonekana kama laana, na watoto hao ili wakubalike katika jamii hiyo, ni lazima wazazi wao wawafanyie sherehe maalum ya kuwatakasa kwa kuchinja ng'ombe na kucheza ngoma.

Esther Namuhisa anaarifu zaidi.