Marais wa Urusi na Uturuki wajadili tofauti kuhusu sera zao juu ya Syria

Rais wa Urusi Vradimir Putin na rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Marais wa Urusi na Uturuki wajadili tofauti zao

Rais wa Urusi Vradimir Putin amesema kuwa inawezekana kumaliza tofauti baina yake na Urusi na Uturuki juu ya sera zao kuhusu Syria.

Akizungumza baada ya mkutano baina yake na rais wa Uturuki mjini St Petersburg, rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan alielezea mazungumzo yao kama yaliyokua mazuri na yenye kuleta faida. Hatua za kiuchumi pia zilijadiliwa.

Safari za ndege za Urusi kuelekea Uturuki zinatarajiwa kufunguliwa tena ambapo chakula kitasafirishwa kutoka Uturuki hadi Urusi.

Hii ilikua ni ziara ya kwanza ya rais Erdogan tangu kufanyika kwa jaribio la mapinduzi dhidi ya serikali yake mjini mwezi uliopita. Uhusiano baina ya nchi hizo mbili uliingia dosari mwaka jana wakati Uturuki ilipoidungua ndege ya Urusi kwenye mpaka wa Syria.