Edorgan na Putin waanza ukurasa mpya wa uhusiano

Baada ya mkutano huo ulofanyika katika mji wa St. Petersburg Urusi, Edorgan na Putin walikubaliana kuzidisha uhusiano wa kiuchumi.
Maelezo ya picha,

Baada ya mkutano huo ulofanyika katika mji wa St. Petersburg Urusi, Edorgan na Putin walikubaliana kuzidisha uhusiano wa kiuchumi.

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Edorgan na Rais wa Urusi Vladmir Putin wamesema kuwa wamefungua ukarasa mpya wa uhusiano wao ambao uliharibika baada ya Uturuki kuangusha ndege ya kivita ya Urusi enelo la mpaka wa Syria mwaka jana.

Baada ya mkutano huo ulofanyika katika mji wa St. Petersburg Urusi, Edorgan na Putin walikubaliana kuzidisha uhusiano wa kiuchumi.

Maelezo ya picha,

Novemba 2015 Uturuki ilidungua ndege za kivita za Urusi katika milima iliyopo Kaskazini mwa nchi hiyo

Hii ndio ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo wa uturuki ndio wa kwanza kufanya ziara nje tangu kushindwa kwa jaribio la mapinduzi.

Edorgan amekua na hasira juu ya washirika wa Magharibi ambao wamekosoa msimamo wake tofauti na msaada wa Putin. Mwandishi wa BBC aliyepo St. Petersburg anasema ni ishara ya umoja baina ya nchi hizo mbili dhidi ya Magharibi.